Mkoa wa Kigoma watia aibu maonyesho ya biashara


KATIKA hali isiyotarajiwa Mkoa wa Kigoma, umesusua kwenye Maonyesho ya Biashara na Fursa za Uwekezaji zilizopo kwenye Ukanda wa Ziwa Tanganyika yanayohusisha Mikoa mitatu ya Katavi, Rukwa na Kigoma, yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwanga Community Center mjini Kigoma. Continue reading

TANGAZO LA NAFASI ZA MASOMO


TANZANIA TRAINING RESEARCH AND OUTREACH CENTRE (TATROC)

MKUU WA CHUO CHA TATROC ANAPENDA KUWATANGAZIA WANAFUNZI NA WAZAZI WOTE KUWA CHUO KIPYA CHA TATROC CHENYE SIFA ZA KIMATAIFA KINATOA KOZI YA MAENDELEO YA JAMII YA MIEZI 9 ITAYOMUANDAA MWANAFUNZI KUAJIRIWA KUWA AFISA MAENDELEO YA JAMII, MTENDAJI WA MTAA/KIJIJI NA KATA, MSHAURI KATIKA MASHIRIKA YA MISAADA.

MWANAFUNZI ATAPATIWA CHETI: “BASIC TECHNICIAN CERTIFICATE IN COMMUNITY DEVELOPME NTA LEVEL 4” AMBACHO KINATAMBULIWA NA SERIKALI, NACTE, WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO PAMOJA NA NGOS.

SIFA KUJIUNGA:

KIDATO CHA NNE, UFAULU KUANZIA D MBILI
FOMU ZA KUJIUNGA:

ZINATOLEWA BURE CHUONI FDC KIHINGA, KIGOMA.
ADA ZETU NI NAFUU SANA NA INALIPWA KWA AWAMU NNE WAHI MAPEMA NAFASI NI CHACHE
MUDA WA KUANZA MASOMO:

TAREHE 1 SEPTEMBA 2015
KWA MAELEZO ZAIDI PIGA SIMU ZIFUATAZO:

O757 – 86 36 83, 0765 – 423 150, 0767 882488 & 0767 – 430 148
KARIBUNI SANA! USIKOSE FURSA HII! CHUO KIPYA KABISA!

By KigomaLive Posted in Elimu

Klabu ya Parma sasa yauza mataji yake


Parma sell their trophies!

 

UKATA ulioikumba klabu ya Parma ya Italia umeilazimisha klabu hiyo kuuza kila kitu ilichonacho.

Na tunaposema “kila kitu”,tunaamanisha “kila kitu”. Klabu hiyo ya Italia imeweka makombe yake yote mnadani katika juhudi za kuinusuru na ukata.

Kulingana na Gazzetta dello Sport, Parma inauza kombe la Coppa d’Italia la mwaka 1992, Kombe washindi la mwaka 1993, UEFA Super Cup la mwaka 1994, UEFA Cups ya mwaka 1995 na 1999 na talian Super Cups ya mwaka 1999 na mwaka 2002.

 

Kauli ya Serikali kuhusu Ebola Kigoma


WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii imefafanua kuwa hakuna uthibitisho kwamba mkimbizi aliyekufa kwenye kambi ya Nyarugusu mkoani Kigoma, alikuwa akiumwa ugonjwa wa Ebola.

Agosti 9 mwaka huu, Buchumi Joel akitokea katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu alipokelewa katika hospitali ya Mkoa wa Kigoma ya Maweni akiwa na dalili za kutokwa na damu sehemu mbalimbali za mwili, hasusan kwenye fizi, macho na masikio. uzikwa chini ya uangalizi wa ofisi ya afya ya mkoa. Continue reading

By KigomaLive Posted in Afya

Mkimbizi adhaniwa kufa kwa Ebola Kigoma


Hivi ndivyo mwili wa mkimbizi kutoka Burundi ulivyozikwa katika makaburi ya Masanga Manispaa ya Kigoma Ujiji, jana jioni.

Hivi ndivyo mwili wa mkimbizi kutoka Burundi ulivyozikwa katika makaburi ya Masanga Manispaa ya Kigoma Ujiji, jana jioni.

MKIMBIZI Raia wa Burundi aliyekuwa akiishi katika Kambi ya Wakimbizi Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma, Buchumi Joel, mwenye umri wa miaka 39 amefariki dunia kutokana na ugonjwa unaodhaniwa kuwa wa jamii ya Ebola akiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kigoma Maweni, usiku wa kuamkia Agosti 10.

Continue reading

By KigomaLive Posted in Habari

Yakufikie matokeo ya kura za maoni CCM Jimbo la Kigoma Kusini


WAGOMBEA wa Kura za Maoni kupitia CCM Jimbo la Kigoma Kusini walikuwa 13.

1.Hasna Mwilima kura 6,063

2.Eng: Salum Sasilo kura 5,501

3.Nashon Bidyanguze kura 3,867

4.Ali Kalufya kura 3,792

5.Manju Salum Msambya kura 3,233

6.Kifu Gulam Husein Shabani kura 2,410

7.Jumanne Husein Mhitila Kalimanzila kura 1,973

8.Norbet Nshemetse kura 1,843

9.Idd Ndabhona kura 1,397

10.January Kizito kura 1,331

11.Waziri Mourice kura 613

12.Dismas Malele kura 443

13.Thomas Sangai kura 79

By KigomaLive Posted in Habari