Waonywa kutowadhuru watafiti


WANANCHI wa Mkoa wa Kigoma, wametahadharishwa kutowadhuru watafiti au kukwamisha kwa namna yoyote utafiti unaofanywa na serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), pamoja na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), kuhusu hali ya upatikanaji wa nishati nchini.

Kuanzaia Octoba 10 mwaka huu, serikali imeanza kufanya utafiti wa kuangalia hali ya upatikanaji wa nishati hususani katika maeneo ya vijijini wa mwaka 2016, utafiti ambao utafanyika katika mikoa yote 26 ya Tanzania bara kwa muda wa siku 25 na utakamilika ifikapo Novemba 15 mwaka huu.

Akizungumza ofisini kwake Meneja wa Takwimu, Ofisi ya Taifa ya Takwimu Mkoa wa Kigoma, Moses Kahero, alitoa wito kwa viongozi wa ngazi zote mkoani Kigoma kuhamasisha wananchi wao kutoa ushirikiano kwa wadadisi pindi watakapofika katika maeneo yao kwa ajili ya kukusanya taarifa za utafiti.

“Mtu yeyote atakayepatikana na hatia ya kuwazuia watafiti kutekeleza majukumu yao ya kitakwimu atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria ya takwimu ya mwaka 2015 kifungu cha 37,”alionya Kahero.

Aidha bw.Kahero, alisema kwa mkoa wa Kigoma, tayari utafiti huo umeanza katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, na baadaye utafanyika katika Wilaya ya Uvinza, kisha kufuatiwa na Wilaya zingine za mkoa huo.

“Utafiti huu utahusisha jumla ya maeneo 26 katika mkoa wetu wa Kigoma yaliyochaguliwa kitaalam na kila eneo zitahojiwa kaya 15 kuwakilisha kaya nyingine katika maeneo hayo,”aliongeza.

Alisema timu ya wadadisi wapatao watano watahusika katika ukusanyaji wa taarifa hizo ambapo kutakuwa na msimamizi mmoja (Meneja Takwimu wa Mkoa), na wataalam wengine kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Makao Makuu.

Lengo la serikali kufanya utafiti huo ni kukusanya takwimu rasmi zinazohusu hali ya upatikanaji wa nishati ya umeme katika ngazi ya jumuiya na kaya na matumizi ya umeme, ambazo zitatumika kuendeleza mipango ya usambazaji wa umeme vijijini kupitia miradi mbali mbali itakayotekelezwa na serikali kwa ajili ya kuongeza wigo wa upatikanaji wa nishati bora vijijini.

Utafiti huo ni wa kwanza kufanyika ukihusisha mikoa yote ya Tanzania bara. Mwaka 2011 ulifanyika utafiti wa awali wa kutathmini hali ya upatikanaji wa nishati nchini ambao ulihusisha baadhi tu ya mikoa ya Tanzania bara.

Hadi Juni mwaka huu upatikanaji wa umeme vijijini ulifikia asilimia 41%, huku katika ngazi ya kitaifa hadi kufikia Juni mwaka huu kiwango cha upatikanaji wa umeme kwa wananchi wa mijini na vijijini kimefikia asilimia 58%.

Advertisements
By KigomaLive Posted in Habari

Toa Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s