Waziri Mwigulu awageukia watendaji wa vijiji


WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh.Mwigulu Nchemba, amewataka watendaji wa Vijiji na Kata kulipatia kipaumbele suala la kuwatambua raia na wahamiaji haramu katika maeneo yao ili kudhibiti vitendo vya uhalifu wa kutumia silaha badala ya kudhani kuwa hilo ni jukumu la polisi pekee.

Amesema hayo wakati wa ziara yake mkoani Kigoma, ambapo alipata nafasi ya kukutana na watendaji wa vijiji na kata kutoka halmashauri ya wilaya ya Kasulu, ambapo amesema watendaji wasidhani kwamba wajibu wao wa utendaji unakomea katika ofisi zao bali wanao pia wajibu wa kulinda usalama.

Aidha Waziri Mwigulu, ameongeza kuwa kiongozi yeyote au mwananchi atakaebainika kuwezesha uingiaji wa wahamiaji haramu katika maeneo yake ataunganishwa kwenye makosa ya uhamiaji haramu.

“Na kwa sasa tunapanga kuwa wakali kweli kweli kwa yeyote ambaye hatatoa ushirikiano kwenye jambo la kutambua wahamiaji haramu,”alisema Waziri Mwigulu.

Mapema kabla ya kukutana na watendaji hao Waziri Mwigulu Nchemba, alipokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Kanali Marco Gaguti na Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Martin Mkisi, ambao walimweleza waziri kuwa hali ya usalama ni nzuri ingawa wamekiri kwamba suala la wahamiaji haramu linaendelea kuwa tishio namba moja la usalama katika maeneo yao.

Advertisements
By KigomaLive Posted in Habari

Toa Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s