Saadani hifadhi ya kipekee


 

  • Nyati baadhi ya vivutio katika hifadhi ya Saadani

    Nyati baadhi ya vivutio katika hifadhi ya Saadani

 

Diana Rubanguka

Saadani.

Imeelezwa kuwa Hifadhi ya Taifa ya Saadani iliyoko Mkoa wa Pwani na Tanga ni hifadhi ya kipekee kutokana na kuwa na aina nne za utalii ndani mwake tofauti na hifadhi nyingine nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari wanawake hifadhini hapo mhifadhi utakii Apaikunda Mungule alisema kuwa upekee huo unatokana na kuwa na aina nne za utalii ndani mwake ambazo ni Utalii wa boti ndani ya mto Wami, utalii wa fukwe za Bahari ya Hindi, utalii wa kutembea kuona wanyama pamoja na utalii wa kuzunguka na gari ili kuona wanyama waliopo hifashini humo.

Mungule alisema kuwa hali hiyo inachangia ongezeko kubwa la watalii ambapo tangu kuanzishwa kwa hifadhi hiyo 2005 idadi ilikua 3758 na kufikua 2015 idadi imekuwa 450,000 hivyo kutoa wito kwa watanzania kujitokeza kutembelea hifadhi hiyo ili kujionea vivutio hivyo vya kipekee.

Awali akisoma taarifa   ofini kwake mbele ya Umoja wa waandishi wa habari wanawake Tanzania (WJT) kaimu mhifadhi mkuu wa hifadhi ya Saadani Lomi Ole Meikasi alisema hifadhi imetumia  fedha za kitanzania zaidi ya shukingi  milioni 722 katika kujenga miradi ya huduma za jamii katika vijiji vinavyo zunguka  hifadhi hiyo kuimalisha ujirani mwema baina ya hifadhi na jamii inayoizunguka.

“Ujirani mwema unatusaidia tupunguza ujangili wa wanyama hifadhini, tumajenga zahanati, tumejenga Vyumba vya madarasa na kuchangia madawati 150,000 katika shule za misingi  za vijiji vya Mkoa wa Tanga na Pwani lakinj pia tumeboresha baadhi ya miundo mbinu ya barabara” alisema Ole Meikasi

Mhifadhi Mikasi alisema kuwa lengo kubwa ni kudumisha mahusiano baina yao na jamii inayozunguka hifadhi kwa kuboresha Huduma za kijamii  ilikuhakikisha hifadhi hiyo inalindwa na  Wananchi kutoa ushirikiano kwa kutoka taarifa kwa wa hifadhi dhidi ya majangili na wavamizi wa hifadhi  unao sababisha Wanyama wengi kuuliwa na kupelekea idadi kubwa ya Wanyama kutoweka Hifadhini humo.

Aidha  alisema kuwa hali hiyo ya ujirani mwema imesaidia kuimalisha ulinzi kutokana na wakazi wanaoishi jirani na hifadhi hiyo kuona umuhimu kutokana na hifadhi kushiriki  katika  kuboresha huduma  za kijamii na ilikuweza kusaidia ulinzi wawanyama na vivutio vilivyopo katika Hifadhi hiyo kutokana na hifadhi hiyo haina uzio wa kuzuia wanyama kutoka nje ya hifadhi

“hifadhi hii ni nzuri Ina wanyama wengi Kama vile Twiga, pundamilia,Tembo na wanyama wengine wengi ikiwa ni pamoja na  kasa anaetokea Nchini India na kuja kutaga mayai yake  katika fukwe za bahari ya Hindi katika hifadhi hivyo ninaamini watalii wakija huku kwenye hifadhi zetu watafurahia Sana”, alieleza mhifadhi utalii.

Alisema kwasasa watalii wote watapokelewa hifadhini hapo wakiwa na kadi za utalii zinazo tolewa na Taasisi za kifedha  zitakazo wasaidia kuingia hifadhini kwa watalii watakao shindwa kuingia na kadi hawataruhusiwa kuingia hifadhini.

Naye Mwenyekiti wa umoja wa waandishi wa habari wanawake Tanzania  (WJT) Esther Macha alilishukuru shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kwa kukubali kutoa ufadhili kwa wanahabari wanawake ili kuweza kutembelea hifadhi za Taifa za TANAPA kwa ajili ya kujifunza  na kutumia kalamu zao kuihamisisha jamii kutembelea hifadhi za Taifa za Tanzania.

Macha aliahidi kuwa wanahabari wanawake watatumia kalamu zao kupitia vyombo vyao vya habari wanavyolipotia kuelimisha jamii umuhimu wa utalii wa ndani badala ya kuwaachia wageni pekee kutembelea hifadhi hiyo na kusema kuwa pamoja na kutembelea hifadhi ya Saadani
Watatembelea pia hifadhi za Udzungwa,mikumi na Luaha.

 

 

Advertisements
By KigomaLive Posted in Habari

Toa Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s