CCM Kigoma watumbuana


HALMASHAURI kuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kigoma, imewafukuza uanachama, wanachama tisa wa chama hicho kutoka wilaya ya Uvinza na wilaya ya kichama ya Kigoma mjini, ambao wanatuhumiwa kukisaliti chama wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Maamuzi ya kuwafuta wanachama hao yamefikiwa katika kikao cha halmashauri kuu ya mkoa kilichoketi jana katika ukumbi wa mikutano wa CCM mkoa wa Kigoma, na kufanya tathimini ya uchaguzi mkuu uliopita chini ya mwenyekiti wake Dkt.Amani Warid Kabourou.

Akitangaza maamuzi hayo, Dkt.Kabourou, ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, amesema waliofutwa uanachama ni Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Uvinza, Josephine Ntahuheza, Katibu mwenezi wilaya ya Uvinza, Majaliwa Zuberi Kayandamila, na mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Uvinza Asha Omary Kiembwe.

Wengine ni Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kigoma Mjini, Asha Omary Ibrahimu, Katibu wa CCM Kata ya Rusimbi Bakari Songoro, Katibu wa CCM Kata ya Kagera, Kana Athumani.

Aidha dkt.Kabourou amesema wengine waliopoteza uanachama wao ndani ya CCM kwa kusatili na kuhama chama kuwa ni Twaha Bishingwa, aliyekuwa mchumi kata ya Rubuga, Damasi, aliyekuwa mwenyekiti wa UVCCM wilaya na Shabani Njoregwa, ambao wote hao wamehamia ACT Wazalendo.

“Huu ni wito wa chama kitaifa tangu mashina, matawi, kata, wilaya na vikao vyote vya chama vilielekezwa vifanye tathimini ya uchaguzi wa mwaka 2015,”alisema Dkt.Kabourou wakati akitangaza hatua hiyo.

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Kigoma, Stanley Mkandawile, alisema vitendo vya usaliti vilivyofanywa na wanachama hao kuwa ni pamoja na kuwafanyia kampeni wagombea wa vyama vingine na kwamba kwa kufanya hivyo walikiuka kanuni ya uongozi na maadili ya chama ibara ya tatu kifungu cha tatu kifungu kidogo cha pili na kifungu cha tatu kifungu kidogo cha tatu.

Nae Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Kigoma, Kalembe Masoud Bakari, alisema usaliti ndani ya Chama cha Mapinduzi Kigoma ni ugonjwa uliokitafuna chama hicho kwa muda mrefu na hakuna hatua zozote zilizokuwa zikichukuliwa.

“Uchaguzi unapofika miongoni mwetu wanakuwepo wasaliti na ugonjwa huu hakuanza leo, ugonjwa huu umeanza miaka 17 iliyopita. CCM haijawahi kushika halmashauri au Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa sababu ya changamoto za viongozi na baadhi ya wanachama kuwa wasaliti wa chama,”alisema Kalembe.

Mmoja wa wanachama waliofukuzwa CCM, Josephine Hosea Ntahuheza, amesema halmashauri kuu ya mkoa imekurupuka kuchukua maamuzi hayo na kwamba yeye hakusaliti chama hivyo atakata rufaa katika ngazi za juu.

 

Advertisements
By KigomaLive Posted in Habari

Toa Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s