Mh.Katimba ataka Chipukizi waandaliwe kuwa viongozi bora


Mh.Zaibab Katimba (MB), akizungumza na Vijana katika mabaraza ya UVCCM Kigoma.

Mh.Zaibab Katimba (MB), akizungumza na Vijana katika mabaraza ya UVCCM Kigoma.

 

MKUU wa Idara ya Chipukizi Sekondari na Vyuo vikuu, Makao Makuu ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Mh.Zainab Katimba, ameagiza kila wilaya mkoani Kigoma ihakikishe inakuwa na ulezi wa chipukizi ili kuwaandaa kuwa viongozi bora hapo baadaye.

Alitoa agizo hilo wakati alipofanya ziara mkoani Kigoma, yenye lengo la kukagua uhai wa jumuiya ya vijana mkoani Kigoma ambapo kwa nyakati tofauti amekutana na mabaraza ya UVCCM katika wilaya za Uvinza na Kigoma pamoja na shirikisho la vyuo vya elimu ya juu.

Sambamba na hilo Mh.Katimba ambaye ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anayetokana na Jumuiya ya UVCCM, aliagiza iandaliwe orodha kamili ya chipukizi wote katika mkoa wa Kigoma, ikiwa ni pamoja na kuandaa vikao vyao kwa mujibu wa kanuni za chipukizi.

Aidha katika ziara hiyo Mh.Katimba, alifanya kazi ya kuzindua shina la wakereketwa la Msufini mjini Kigoma, na kufanikiwa kuingiza wananchama wapya 300 wa UVCCM.

 

Baadhi ya Vijana wa UVCCM KIgoma, wakimsikiliza Mh.Katimba alipofanya ziara mkoani Kigoma na kukutana na mabaraza ya UVCCM.

Baadhi ya Vijana wa UVCCM KIgoma, wakimsikiliza Mh.Katimba alipofanya ziara mkoani Kigoma na kukutana na mabaraza ya UVCCM.

Wakati huo huo Mh.Katimba, ametekeleza ahadi yake kwa jumuiya ya UVCCM mkoa wa Kigoma ya kuwanunulia vitendea kazi kwa ajili ya ofisi za umoja wa vijana kila wilaya ambapo amekabidhi laptop 8 ili kuboresha utendaji wa shughuli zao.

Katika hatua nyingine Mh.Katimba, aliwakumbusha vijana kuwa ‘siasa na uchumi’ ni pande mbili za sarafu moja hivyo kuagiza kuitishwa baraza maalum la vijana litakaloshirikisha wakufunzi wa masuala ya ujasiriamali na utambuzi wa fursa zinazowazunguka vijana na kuwataka vijana kujikita katika kujielimisha na kutumia fursa zinazowekwa na serikali kujikwamua kiuchumi.

“Fursa za kujiimarisha zipo nyingi ni sisi wenyewe kuzitafuta,”alisisitiza Mh.Katimba.

 

Mh.Zainab Katimba, katika picha ya pamoja na wakereketwa muda mfupi baada ya kuzindua shina la wakereketwa la Msufini.

Mh.Zainab Katimba, katika picha ya pamoja na wakereketwa muda mfupi baada ya kuzindua shina la wakereketwa la Msufini.

 

Awali katika mabaraza hayo pia vijana walipata nafasi ya kueleza dukuduku zao kuhusiana na tatizo la ajira na kuulalamikia uongozi wa CCM wilaya ya Kigoma kwa kuwatelekeza baada ya uchaguzi licha ya kufanya kazi mchana na usiku kukipigania chama ili kipate ushindi.

Pia waliwashutumu viongozi wasaliti wa chama katika uchaguzi mkuu uliopita na kusababishwa jimbo la Kigoma mjini kutwaliwa na upinzani.

Akizungumzia malalamiko ya vijana hao kuhusiana na kutelekezwa baada ya uchaguzi, Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Mrisho Gambo, aliyeambatana na Mh.Katimba katika ziara hiyo, alionya kuwa chama kisipokuwa makini kitaadhibiwa ikiwa vijana watapuuzwa.

Advertisements
By KigomaLive Posted in Habari

Toa Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s