‘Teleza’ awanyima usingizi wanawake Kigoma


WANAWAKE wakazi wa mji wa Kigoma, wamekumbwa na taharuki kufuatia kuibuka mtu asiyefahamika anayewaingilia kinguvu wakati wamelala kwenye nyumba zao usiku huku akitumia panga kuwatisha na kuwakata kata mapanga sehemu mbali mbali za miili yao wale wanaokataa kutekeleza matakwa yake.

Mpaka sasa zaidi ya wanawake 10 wanaelezwa kuvamiwa na mtu huyo ambaye kwa sasa ni maarufu kwa jina la Teleza, kwani inaelezwa kuwa hujipaka mafuta ya mawese ili mwili wake uteleze na asiweze kukamatwa kirahisi na inadaiwa kuwa huwafuata Zaidi wanawake wasio na waume huku akitumia kisu kuharibu vitasa vya milango kabla ya kuingia ndani.

Tukio la hivi karibuni ni la juzi Mei 24 ambapo msichana mwenye umri wa miaka 20 mkazi wa mtaa wa Mwanga Vamia akiwa amelala chumbani kwake aliingiliwa kimwili na mtu huyo majira ya saa kumi na moja alfajiri ambapo baadhi ya wanawake walioambulia kukaktwa mapanga wamesimulia huku wakishutumu jeshi la polisi kwa kutochukua hatua.

“Hili suala tumekuwa kama vile hatuna uongozi, wanawake tunaonewa, wanawake tunadhalilishwa,”alisema mmoja wa  wanawake waliokumbwa na kadhia hiyo.

Mama mwingine mwenye umri wa miaka 55 ambaye alisema yeye alishafuatwa Zaidi ya mara nne na ‘Teleza’ kwa nia ya kutaka kumbaka, alilalamika kufanyiwa vitendo hivyo na mtoto anaeweza kumzaa na kutaka viongozi wanawake kuingilia suala hilo na kutetea haki za wanawake.

Kwa mujibu wa wananchi suala hilo liliwahi kujitokeza mwaka jana na baadaye kupotea lakini katika kipindi cha wiki mbili sasa limeanza kujirudia na kuleta hofu kubwa miongoni mwa wanawake wa mji wa Kigoma.

Mwanzo suala hilo lilihusishwa na Imani za kishirikina, lakini Diwani wa Kata ya Mwanga Kusini ambayo wanawake wengi wameathiriwa na jambo hilo, Musa Maulidi, amesema wamebaini kuwa ni vijana wahuni tu waliokosa maadili.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui, amethibitisha taarifa za matukio hayo na kusema kuwa awali suala hilo lilikuwa bado halijaripotiwa kwa jeshi la polisi huku akieleza kuwa tayari mtu mmoja amekamatwa na anaendelea kuhojiwa.

“Dhana iliyojengeka mitaani ya kuhusihanisha na masuala ya kishirikina ni dhana potofu kwani wahalifu hao ni kama wahalifu wengine halihusiani na masuala ya uchawi,”alisema Kamanda Mtui.

 

Advertisements
By KigomaLive Posted in Habari

3 comments on “‘Teleza’ awanyima usingizi wanawake Kigoma

Toa Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s