Mwalimu ajiua kwa kujinyonga


Pichani ni askari polisi akifungua kamba zilizotumiwa na marehemu kujinyonga.

Pichani ni askari polisi akifungua kamba zilizotumiwa na marehemu kujinyonga.

 

Vilio na simanzi vimetawala mapema asubuhi ya leo nyumbani kwa Shiza Athumani, mkazi wa Katubuka, baada ya Mwalimu wa shule ya Msingi Buzebazeba katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, Victoria Wiso, mwenye umri wa miaka 38 ambaye ni mke wake kukutwa amejiua kwa kujinyonga kwa kamba jikoni nyumbani kwake alfajiri ya leo.

Watu mbali mbali wakiwemo majirani wamekusanyika mapema asubuhi katika nyumba hiyo huku simanzi ikighubika kila mtu aliyefika eneo hilo na kila mmoja akionekana kustaajabu na wengine walionekana katika makundi wakizungumza hili na lile kuhusiana na tukio hilo.
Wachache tu walibahatika kuona mwili wa marehemu akiwemo mume wake Shiza Athumani, mpaka pale Polisi baadaye walipofika na kuutoa mwili wake kwenye kitanzi kisha kuupeleka chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya mkoa wa Kigoma, Maweni.
Mume wa marehemu Shiza Athumani, amesema alishituka usiku majira ya saa kumi na kukuta mkewe hayumo chumbani walipokuwa wamelala na baada ya kimya kirefu aliamka na kuanza kumtafuta huku akiita jina lake bila mafanikio lakini baadaye aligundua kuwa hata mlango wa nyumba ulifungwa kwa nje.
“Mimi kwa kweli sijui chochote, nimeamka tu saa kumi na mojaa simuoni mke wangu, nafungua mlango, umefungwa kwa nje, nikaamua nivunje mlango,”alisema mume wa marehemu.
Amesema baada ya kuvunja mlango yeye na mpangaji wake walianza kumtafuta lakini hawakumuona na baadaye akatoa taarifa kwa majirani ambao walishirikiana kumtafuta ndipo wakamkuta jikoni akiwa amening’inia kajinyonga.
Ameongeza kuwa hakuwa na ugomvi na mke wake na wala hakukuwa na tatizo lolote kati yao. Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Ferdnand Mtui, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa uchunguzi unafanyika ili kubaini chanzo cha marehemu kujinyonga.
Baadhi ya majirani akiwemo Honorata Sungura, wameelezea kushitushwa na tukio hilo.
Advertisements
By KigomaLive Posted in Habari

Toa Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s