Mke na Mume wauawa kikatili kwa imani za kishirikina


WATU wawili wa familia moja mke na mume, ambao ni Nyanda Masele na Kwilabya Masasila, wakazi wa Kitongoji cha Mawasiliano katika Kijiji cha Mpeta Wilaya ya Uvinza, mkoani Kigoma, wameuawa kwa kukatwa mapanga na watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wa kukodiwa kwa ajili ya kufanya mauaji hayo.

Kwa mujibu wa mtoto wa kike wa marehemu Ngolo Yanda, Tukio hilo limetokea majira ya saa sita usiku wa kuamkia Machi 9 mwaka huu katika kitongoji hicho ambapo majambazi hao walivamia chumbani kwa wazazi wake wakati yeye akiwa amelala chumba kingine na kuwakata kata mapanga na kuwaua.

“Nilisikia mlango unagongwa kwa nguvu na nikasikia kelele na sauti ya mama inaita, ngolo..ngolo njoo unisaidie, halafu nikasikia sauti nyingine ikisema tulia wewe na tukawa tunaona tochi zinamulika ndani,”alisema mtoto wa marehemu.

Alisema kuwa baada ya muda ikawa kimya ndipo akatoka chumbani kwake na alipokwenda chumbani kwa wazazi wake alikuta wote wako chini na damu zimetapakaa ndani na kwenye miili yao akapiga kelele na kwenda kumuita kaka yake aliyelala nyumba nyingine.

Mtoto wa kiume wa marehemu Juma Nyanda, amesema wakati yeye na watu wengine wanaamka baada ya kugongewa mlango na dada yake, walikuta majambazi hao wameondoka na ndipo wakapiga kelele na majirani kukusanyika na kuanza kuwafuatilia bila mafanikio.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mpeta, Raphael John, amesema chanzo cha tukio hilo lililoleta simanzi kijijini hapo ni imani za kishirikina kwani watu hao baada ya kukamatwa na askari wa kituo cha Nguruka, wamekiri kuwa walikodiwa na mke mdogo wa marehemu Salome Igede kwa shilingi laki sita ili kufanya mauaji hayo.

“Walijieleza kuwa walikuwa wamekubaliana malipo ya laki sita na mke mdogo wa marehemu ambaye alimtuhumu mke mwenzie kuwa alikuwa anamroga kwa muda mrefu na kwamba aliwahi kuhangaika na mimba isiyozalika kwa muda wa miaka kumi,”alisema Mwenyekiti huyo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma, Ferdnand Mtui, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema watu watano wanashikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo wakiwemo mke mdogo wa marehemu na mtoto wa marehemu anaedaiwa kushirikiana na mama yake kula njama ya mauaji.

Advertisements
By KigomaLive Posted in Habari

3 comments on “Mke na Mume wauawa kikatili kwa imani za kishirikina

  1. WATU WA MKOA WAKIGOMA TUSIWE MAKATILI KIASI CHAKUUANA HIVI KIKUBWA TUPENDANE KAMA NDUGU WAFAMILIA MOJA.

Toa Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s