Miili ya Askari wa JKT Bulombora waliofariki katika ajali yaagwa

Katibu Tawala wa mkoa Kigoma Injinia John Ndunguru (kushoto) akiongoza kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kigoma kuaga miili ya vijana wa jeshi la kujenga Taifa waliofariki kwenye ajali ya gari juzi nje kidogo ya manispaa ya kigoma ujiji vijana hao wamesafirisha jana kuelekea makwao kwa taratibu za mazishi.

Mkuu wa kambi ya JKT Bulombora kikosi cha 821 Luteni Kanali Mohamed Mketo (kushoto) akitoa heshima kwa vijana wa JKT waliofariki kwa ajali ya gari mkoani Kigoma juzi ambapo vijana hao walisafirishwa jana kuelekea kwenye mikoa yao kwa mazishi.

Baadhi ya wanajeshi wa jeshi la wananchi wa Tanzania na wapiganaji kutoka JKT Bulombora wakitoa heshima kuaga miili ya vijana wa JKT waliofariki kwa ajali ya gari juzi mjini Kigoma.

Baadhi ya wanajeshi wa jeshi la wananchi wa Tanzania na wapiganaji kutoka JKT Bulombora wakitoa heshima kuaga miili ya vijana wa JKT waliofariki kwa ajali ya gari juzi mjini Kigoma.

(Picha na Fadhil Abdallah).

KATIBU Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Eng. John Ndunguru, leo mchana amewaongoza waombolezaji kuaga miili ya askari saba wa Jeshi la Kujenga Taifa Kikosi cha 821KJ Kambi ya Bulombora mkoani Kigoma, ambao wamefariki dunia jana katika ajali ya gari.

Akiongea kwa niaba ya serikali wakati wa kuaga miili ya askari hao ambao wawili kati yao walikuwa askari wa kudumu na watano wa kujitolea, John Ndunguru, ametoa pole kwa wafiwa wote sambamba na kuwataka wananchi pamoja na uongozi wa jeshi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha majonzi.

Kabla ya miili ya askari hao kusafirishwa, Mkuu wa Vikosi vya Jeshi mkoani Kigoma Kanali Mamdali Msuya, kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania,ametoa shukrani kwa watu wote walioungana na jeshi baada ya tukio hilo vikiwemo vikosi mbali mbali vya majeshi na Hospitali ya Maweni.

Ajali hiyo ilitokea jana jioni majira ya saa kumi na nusu katika kijiji cha Kasaka eneo la mzani, wakati askari hao wakisafiri kutoka kikosini Bulombora kwenda mjini Kigoma kikazi kwa kutumia gari lenye namba 57117 JW 09 mali ya jeshi, ambalo lilipasuka tairi zote za nyuma na kupoteza uelekeo.

IMG-20151002-WA0002

IMG-20151002-WA0006

Askari waliofariki dunia katika ajali hiyo ni MT 54407 Sajenti Ally Hamidu Kambanga na MT 108155 Abel Tadei Maisha ambao walikuwa askari wa kudumu na wengine AH 6831 SM (Service Man), Eugine Stephano Butati, AH 7190 SM Said Sadala Said, REC (Recruit) Abubakar Salum Washokera, REC Bakari Ramadhani Kibaya na REC Frederick Kahemela Ephrahim.

Askari wengine 22 ambao wamejeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma, Maweni, kufuatia ajali hiyo, wametajwa kuwa ni Benedicto Ndokeye, Raphael Kibamba, Antanas Emmanuel, Abuu Nzoghe Hassan, Abubakar Mathias Peter, Bakari Sinuki Mwaisunga, Deus Manyanya Charles, Peter Edward Nyanda, Elias Masaga Magesa, Geofrey Peter Malik na King Lucas Kasofu.

Wengine ni Camilius William Hagida, Lameck John, Martin Andrew Lupatu, Steven Denis Mtege, Said Omary Kitogo, Said Suleiman Zuberi, Shabani Idd Zakaria, Victor Adelbert, Jackson John Nyarubi, Mohamed Jackson Nyimbo na Abubakar Hassan Mkubi, ambao kulingana na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dr.Fadhil Kibaya wengi hali zao zinaendelea vizuri..

Toa Maoni Yako Kuhusu Habari Hii