Jimbo Katoliki Kigoma lapata Askofu Mpya


E80A6465

KANISA Katoliki Jimbo la Kigoma limepata Askofu mpya, kufuatia kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Mhashamu Askofu Joseph Mlola, kuwa Askofu mpya wa Jimbo hilo.

Kabla ya kuwekwa wakfu hati ya uteuzi kutoka kwa Papa Benidikto wa 16, ilisomwa na Balozi wake hapa nchini Francisco Montecillo Padilla, ambaye alisoma hati hiyo kwa lugha ya Kilatini.

Katika salaam za Serikali kwa Kanisa Katoliki, Jimbo la Kigoma, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, licha ya kumpongeza Askofu Mlola kuteuliwa kuongoza jimbo hilo, ameeleza kutambua mchango wa madhehebu ya Dini likiwemo Kanisa Katoliki kwa Jamii ya Watanzania.

Akitoa salaam hizo kwa niaba ya Rais, kwenye ibada ya kupewa Daraja la Uaskofu kwa Askofu Mlola, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Maalum, Mark James Mwandosya, amesema mchango wa Kanisa Katoliki katika huduma mbali mbali za kijamii utalisaidia Taifa kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025.

“Madhehebu ya dini yamechangia kwa kiwango kikubwa katika kuendeleza elimu na huduma nyingine za jamii hasa afya,”alisema.
“Tumethamini mchango wenu na ushauri wenu katika masuala yanayomgusa mwananchi hata pale Baba Maaskofu wakati mwingine ujumbe mliotutumia ulitufikia kwa maneno makali. Mchango wenu hasa katika maeneo ya elimu na afya hakika utatusaidia kuyafikia malengo yaliyo katika dira ya Taifa 2025.”

Awali akiongea wakati wa kumkabidhi Askofu Mlola, hatamu za uongozi wa Jimbo la Kigoma, Baba Askofu Mkuu wa Jimbo la Tabora, Paulo Ruzoka, ambaye pia alikuwa msimamizi wa Jimbo la Kigoma,alieleza huduma za kijamii ambazo zimekuwa zikitolewa na Jimbo hilo.

Alisema Jimbo lina shule za Sekondari 8, shule za msingi 2, vituo vya mafunzo stadi mbali mbali na kituo kimoja cha chekechea pamoja na kutoa huduma kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira maagumu.

Nae Balozi wa Papa hapa nchini Fransisco Padilla, amemuasa Askofu mpya wa Jimbo la Kigoma, kuutangaza ukweli ambapo pia amewaomba Mapadri, Masista na waamini wote watoe ushirikiano kwa ajili ya mustakabali mwema wa Jimbo la Kigoma na Kanisa kwa ujumla.

Akitoa salaam za Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Rais wa Baraza hilo, Mhashamu Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, amemkaribisha katika umoja wa baraza hilo ambapo alisema atakuwa chachu ya utendaji na kwamba mchango wake unahitajika katika kulijenga kanisa na taifa la Tanzania.

Kwa upande wake Askofu mpya wa Jimbo la Kigoma, Mhashamu Askofu Joseph Mlola,alisema kuwa sala za waumini, upendo na ushirikiano wao ndio nguvu ya pekee itakayomsaidia kufanya utume alioupokea.

Jimbo Katoliki la Kigoma limekuwa bila Askofu tangu mwaka 2012, kufuatia Papa Benedikto wa 16 kumteua aliyekuwa Askofu wa Jimbo hilo Protas Rugambwa, kuwa Katibu Mwambata Idara ya uenezaji Injili, ambapo waumini wameeleza furaha yao kwa kumpata Askofu.

Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Kigoma, Mhashamu Askofu Joseph Mlola, katika picha kumbukumbu na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Maalum, Prof.Mark Mwandosya kulia na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya.

Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Kigoma, Mhashamu Askofu Joseph Mlola, katika picha kumbukumbu na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Maalum, Prof.Mark Mwandosya kulia na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya.

Advertisements

Toa Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s