Goli la mchezaji Charles Timothy katika dakika ya 78 limewapa ushindi JKT Kanembwa kwenye mchezo wa kiporo cha mzunguko wa kwanza wa Ligi Daraja la Kwanza dhidi ya Stand United ya Shinyanga uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi Mjini Tabora.
Tazama matukio mbali mbali ya mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza kati ya JKT Kanembwa na Stand United kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi Mjini Tabora.

Eneo la Jukwaa kuu la uwanja wa Ally Hassan Mwinyi Mjini Tabora likiwa limefurika mashabiki waliofika kushuhudia mchezo huo

Askari wa Kikosi cha kutuliza Ghasia FFU akishuka kwa unyonge baada ya kwenda eneo la mashabiki wa JKT Kanembwa waliokuwa wakishangilia kwa vurugu ili kuwatia adabu, lakini baada ya Bosi kutoka JKT kufika eneo hilo akaamriwa ashuke.